Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya:
“Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu,
yanyoosheni mapito yake.
Kila bonde litajazwa,
kila mlima na kilima vitashushwa.
Njia zilizopinda zitanyooshwa,
na zilizoparuza zitasawazishwa.
Nao watu wote watauona
wokovu wa Mungu.’”