Kisha ibilisi akampeleka hadi Yerusalemu, akamweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa, kwa maana imeandikwa:
“ ‘Atakuagizia malaika wake
ili wakulinde kwa uangalifu;
nao watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’”
Isa akamjibu, “Imenenwa: ‘Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’”