Mattayo MT. 3

3
1SIKU zile akaondokea Yohana Mbatizaji akikhubiri katika jangwa ya Yahudi, akinena, 2Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,
Sauti yake apigae mbin jangwani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Nyosheni mapito yake.
4Yohana mwenyewe alikuwa na mavazi yake ya singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.
5Ndipo wakamwendea Yerusalemi, na Yahudi yote, na inchi zote za kando za Yordani; 6wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao. 7Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo? 8Zaeni bassi matunda yaipasayo toba; 9msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto. 10Nalo shoka limekwisha kuwekwa penye shina la miti; bassi killa mti usiozaa matunda mazuri unakatwa na kutupwa motoni. 11Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
13Ndipo Yesu akafika hatta Yordani kwa Yohana kutoka Galilaya illi abatizwe nae. 14Lakini Yohana alikuwa akimzuia, akinena, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, na wewe waja kwangu? 15Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha. 16Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake: 17na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.

اکنون انتخاب شده:

Mattayo MT. 3: SWZZB1921

های‌لایت

به اشتراک گذاشتن

کپی

None

می خواهید نکات برجسته خود را در همه دستگاه های خود ذخیره کنید؟ برای ورودثبت نام کنید یا اگر ثبت نام کرده اید وارد شوید