Luka 13:18-19
Luka 13:18-19 SRB37
Kisha akasema: Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Niufananishe na nini? Umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukitupia shambani kwake. Nacho hukua na kupata kuwa mti, hata ndege wa angani hutua katika matawi yake.