Mathayo 1
1
Ukoo wa Yesu
(Lk 3:23-38)
1Hii ni historia ya ukoo wa Yesu, Masihi.#1:1 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Kristo”, tafsiri ya Kiyunani kwa neno “Masihi”. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno. Pia katika mstari wa 16-17 na katika kitabu chote hiki. Alitoka katika ukoo wa Daudi, aliyetoka katika ukoo wa Abrahamu.
2Abrahamu alikuwa baba yake Isaka.
Isaka alikuwa baba yake Yakobo.
Yakobo alikuwa baba wa Yuda na ndugu zake.
3Yuda alikuwa baba wa Peresi na Zera. (Mama yao alikuwa Tamari.)
Peresi alikuwa baba yake Hezroni.
Hezroni alikuwa baba yake Ramu.
4Ramu alikuwa baba yake Aminadabu.
Aminadabu alikuwa baba yake Nashoni.
Nashoni alikuwa baba yake Salmoni.
5Salmoni alikuwa baba yake Boazi. (Mama yake Boazi alikuwa Rahabu.)
Boazi alikuwa baba yake Obedi. (Mama yake Obedi alikuwa Ruthu.)
Obedi alikuwa baba yake Yese.
6Yese alikuwa baba yake Mfalme Daudi.
Daudi alikuwa baba yake Sulemani. (Mama yake Sulemani alikuwa mke wa Uria.)
7Sulemani alikuwa baba yake Rehoboamu.
Rehoboamu alikuwa baba yake Abiya.
Abiya alikuwa baba yake Asa.
8Asa alikuwa baba yake Yehoshafati.
Yehoshafati alikuwa baba yake Yoramu.
Yoramu alikuwa baba yake Uzia.
9Uzia alikuwa baba yake Yothamu.
Yothamu alikuwa baba yake Ahazi.
Ahazi alikuwa baba yake Hezekia.
10Hezekia alikuwa baba yake Manase.
Manase alikuwa baba yake Amoni.
Amoni alikuwa baba yake Yosia.
11Yosia alikuwa baba wa Yekonia#1:11 baba wa Yekonia Mfalme Nebukadneza aliuangusha mji wa Yerusalemu na kuvunja hekalu mwaka 586 KK na kuwapeleka Babeli wakiwa mateka watu Mashuhuri pamoja na vyombo vya thamani vilivyokuwa hekaluni. Tazama 1 Nya 3:15-16. na ndugu zake.
Walioishi wakati ambao watu walipelekwa utumwani Babeli.
12Baada ya uhamisho wa Babeli,
Yekonia akawa baba yake Shealtieli.
Shealtieli alikuwa babu wa Zerubabeli.
13Zerubabeli alikuwa baba yake Abiudi.
Abiudi alikuwa baba yake Eliakimu.
Eliakimu alikuwa baba yake Azori.
14Azori alikuwa baba yake Sadoki.
Sadoki alikuwa baba yake Akimu.
Akimu alikuwa baba yake Eliudi.
15Eliudi alikuwa baba yake Eliazari.
Eliazari alikuwa baba yake Matani.
Matani alikuwa baba yake Yakobo.
16Yakobo alikuwa baba yake Yusufu,
Yusufu alikuwa mume wa Mariamu.
Na Mariamu alimzaa Yesu, anayeitwa Masihi.
17Kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Abrahamu mpaka kwa Daudi. Na kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Daudi mpaka wakati wa uhamisho wa Babeli. Na palikuwa na vizazi kumi na nne tangu uhamisho wa Babeli mpaka wakati alipozaliwa Yesu, Masihi.
Kuzaliwa kwa Yesu, Masihi
(Lk 2:1-7)
18Kuzaliwa kwa Yesu Masihi, kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa amechumbiwa na Yusufu. Kabla hawajaoana, Yusufu aligundua kuwa Mariamu alikuwa mja mzito. (Yeye alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.) 19Kwa kuwa Yusufu alitaka kufanya kile kilichokuwa, alikusudia kumwacha Mariamu kwa siri bila ya kumvunjia heshima.
20Lakini baada ya Yusufu kuliwazia jambo hili, Malaika wa Bwana alimjia katika ndoto na akamwambia, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako. Mimba aliyonayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21Atamzaa mwana, nawe utamwita Yesu.#1:21 Yesu Jina la Yesu maana yake “Bwana anayeokoa”. Utampa jina hilo Yesu kwa sababu yeye atawaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
22Haya yote yalitokea ili kutimiza maneno ambayo Bwana aliyasema kupitia kwa nabii aliposema:
23“Sikiliza! Msichana bikira atapata mimba
na atazaa mwana.
Huyo watampa jina la Imanueli.”#Isa 7:14
(Yaani “Mungu yu pamoja nasi”.)
24Yusufu alipoamka alifanya kama alivyoelekezwa na Malaika wa Bwana. Alimuoa Mariamu. 25Lakini hakukutana naye kimwili mpaka Mariamu alipomzaa mwana. Na Yusufu akamwita Yesu.
Trenutno odabrano:
Mathayo 1: TKU
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li svoje istaknute stihove spremiti na sve svoje uređaje? Prijavi se ili registriraj
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

: