1
Yn 4:24
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Konpare
Eksplore Yn 4:24
2
Yn 4:23
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Eksplore Yn 4:23
3
Yn 4:14
walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Eksplore Yn 4:14
4
Yn 4:10
Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
Eksplore Yn 4:10
5
Yn 4:34
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
Eksplore Yn 4:34
6
Yn 4:11
Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai?
Eksplore Yn 4:11
7
Yn 4:25-26
Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
Eksplore Yn 4:25-26
8
Yn 4:29
Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?
Eksplore Yn 4:29
Akèy
Bib
Plan yo
Videyo