1
Yohana 14:27
Neno: Maandiko Matakatifu
Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
Összehasonlít
Fedezd fel: Yohana 14:27
2
Yohana 14:6
Isa akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
Fedezd fel: Yohana 14:6
3
Yohana 14:1
Isa akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia.
Fedezd fel: Yohana 14:1
4
Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho wa Mwenyezi Mungu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Fedezd fel: Yohana 14:26
5
Yohana 14:21
Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
Fedezd fel: Yohana 14:21
6
Yohana 14:16-17
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.
Fedezd fel: Yohana 14:16-17
7
Yohana 14:13-14
Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.
Fedezd fel: Yohana 14:13-14
8
Yohana 14:15
“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.
Fedezd fel: Yohana 14:15
9
Yohana 14:2
Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Naenda kuwaandalia makao.
Fedezd fel: Yohana 14:2
10
Yohana 14:3
Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo.
Fedezd fel: Yohana 14:3
11
Yohana 14:5
Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?”
Fedezd fel: Yohana 14:5
Kezdőoldal
Biblia
Olvasótervek
Videók