1
Luka 13:24
Neno: Maandiko Matakatifu
Isa akawaambia, “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza.
Összehasonlít
Fedezd fel: Luka 13:24
2
Luka 13:11-12
Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, “Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako.”
Fedezd fel: Luka 13:11-12
3
Luka 13:13
Isa alipomwekea mikono yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu.
Fedezd fel: Luka 13:13
4
Luka 13:30
Tazama, kunao walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, nao wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.”
Fedezd fel: Luka 13:30
5
Luka 13:25
Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’
Fedezd fel: Luka 13:25
6
Luka 13:5
Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo.”
Fedezd fel: Luka 13:5
7
Luka 13:27
“Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’
Fedezd fel: Luka 13:27
8
Luka 13:18-19
Kisha Isa akauliza, “Ufalme wa Mwenyezi Mungu unafanana na nini? Nitaufananisha na nini? Umefanana na punje ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake. Nayo ikakua, ikawa mti nao ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Fedezd fel: Luka 13:18-19
Kezdőoldal
Biblia
Olvasótervek
Videók