Mwanzo 11
11
Mnara wa Babeli
1 #
Mdo 2:6
Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2#Dan 1:2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4#Kum 1:28; Yn 5:44; Lk 1:51 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5#Mwa 18:21; Zab 33:13; 53:2 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6#Zab 2:1,4 BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7#Mwa 1:26; 42:23; Kum 28:49; Yer 5:15; Mdo 2:4-11; 1 Kor 14:2,11,23 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8#Mwa 10:25-32; Zab 92:9; Mit 19:29; Lk 1:51 Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9#1 Kor 14:23 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Wazawa wa Shemu
10 #
1 Nya 1:17-27
Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia moja akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika. 11Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
12 #
Lk 3:35
Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. 13Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
14Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi. 15Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
16 #
1 Nya 1:19
Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
18Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu. 19Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike. 20Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
22Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori. 23Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
24Nahori akaishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. 25Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
26 #
Mwa 12:1; Yos 24:2; 1 Nya 1:26 Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani.
Wazawa wa Tera
27 #
Mwa 12:4; 13:10; 14:12; 19:1,29; 2 Pet 2:7 Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. 28Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. 29#Mwa 17:15; 22:20 Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska. 30#Mwa 16:1 Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. 31#Neh 9:7; Mdo 7:4; Ebr 11:8; Mwa 10:19 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. 32Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.
Jelenleg kiválasztva:
Mwanzo 11: RSUVDC
Kiemelés
Megosztás
Másolás
Szeretnéd, hogy a kiemeléseid minden eszközödön megjelenjenek? Regisztrálj vagy jelentkezz be
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.