Mwanzo 6
6
Uovu wa wanadamu
1 #
Ayu 1:6; 2:1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2#2 Kor 6:18; Kum 7:3,4 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua. 3#Lk 19:42; Gal 5:16,17; 1 Pet 3:20; Zab 78:39 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini. 4#Hes 13:33 Nao Wanefili#6:4 Wanefili: maana yake ni majitu. walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. 5#Rum 1:28-31; Mwa 8:21; Kum 29:19; Mit 6:18; Mt 15:19; 24:37; Lk 17:26; 1 Pet 3:20 BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 6#Hes 23:19; 1 Sam 15:11,29; Isa 63:10; Efe 4:30 BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba. 8#Mwa 19:19; Kut 33:12; Lk 1:30; Mdo 7:46 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
Nuhu atengeneza safina
9 #
2 Pet 2:5
Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu. 10Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi. 11Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. 12#Zab 14:2; 33:13 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mtu duniani amepotoka.
13 #
Eze 7:2; Amo 8:2; 1 Pet 4:8 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia. 14Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu. 16Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu. 17#2 Pet 2:5; Rum 5:12,14 Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa. 18Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe. 19Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke. 20Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako ili uwahifadhi. 21#Mwa 1:29,30 Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao. 22#Ebr 11:7; Mwa 7:5 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
Jelenleg kiválasztva:
Mwanzo 6: RSUVDC
Kiemelés
Megosztás
Másolás
Szeretnéd, hogy a kiemeléseid minden eszközödön megjelenjenek? Regisztrálj vagy jelentkezz be
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.