1
Yohana 12:26
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
Confronta
Esplora Yohana 12:26
2
Yohana 12:25
Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele.
Esplora Yohana 12:25
3
Yohana 12:24
Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa, huzaa mbegu nyingi.
Esplora Yohana 12:24
4
Yohana 12:46
Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
Esplora Yohana 12:46
5
Yohana 12:47
“Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
Esplora Yohana 12:47
6
Yohana 12:3
Kisha Mariamu akachukua chupa ya painti moja yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
Esplora Yohana 12:3
7
Yohana 12:13
Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” “Amebarikiwa mfalme wa Israeli!”
Esplora Yohana 12:13
8
Yohana 12:23
Isa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
Esplora Yohana 12:23
Home
Bibbia
Piani
Video