Logo YouVersion
Icona Cerca

Mattayo MT. 6

6
1ANGALIENI msitoe sadaka zenu mbele ya watu, kusudi mtazamwe nao: kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. 3Bali wewe utoapo sadaka, hatta mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kuume ufanyalo; 4sadaka yako iwe kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri.
5Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri. 7Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8Bassi msifanane na hawo; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 9Bassi ninyi salini hivi;
Baba yetu nliye mbinguni, jina lako takatifu litukuzwe, 10Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11Utupe leo riziki zetu. 12Utusamehe deni zetu, kama sisi tunavyowasamehe wadeni wetu. 13Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu. 14Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi. 15Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
16Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. 17Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe nso; 18illi usionekane na watu kuwa unafunga, bali na Baba yako aliye kwa siri; na Baba yako, aonae kwa siri, atakujazi kwa dhahiri.
19Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba: 20bali jiwekeeni hazina mbinguni, zisikobaribu nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala kuiba; 21kwa maana ilipo hazina yenu, ndipo utakapokuwa na moyo wako. 22Taa ya mwili ni jicho; bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23Lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Bassi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, giza gani hilo!
24Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona. 25Kiva sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni au mnyweni; wala mwili wenu, mvaeni. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa anga, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni awalisha hawo. Ninyi je! si bora kupita hawo? 27Yupi katika ninyi awezae kwa kusumbuka kujiongeza kimo chake mkono mmoja? 28Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini khabari za maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayatendi kazi, wala hayasokoti: 29lakini nawaambieni, ya kwamba hatta Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja la hayo. 30Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31Msisumbuke, bassi, mkinena, Tuleni? au, Tunyweni? au, Tuvaeni? 32Kwa maana haya yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji haya yote. 33Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa. 34Bassi msisumbukie kesho; kwa kuwa kesho itayasumbukia mambo yake.
Watosba kwa siku ubaya wake.

Attualmente Selezionati:

Mattayo MT. 6: SWZZB1921

Evidenziazioni

Condividi

Copia

None

Vuoi avere le tue evidenziazioni salvate su tutti i tuoi dispositivi?Iscriviti o accedi