1 Mose 2
2
Siku ya mapumziko.
1Ndivyo, zilivyomalizika kuumbwa mbingu na nchi na vikosi vyao vyote.#Yoh. 5:17; Ebr. 4:4,10. 2Siku ya saba Mungu alipozimaliza kazi zake zote, alizozifanya, akazipumzikia siku ya saba hizo kazi zake zote, alizozifanya; 3kwa hiyo Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alizipumzikia kazi zake zote, alizozifanya za kuumba.#2 Mose 20:8-11.
Paradiso.
4Hivyo ndivyo, mbingu na nchi zilivyopata kuwapo hapo, zilipoumbwa. Siku hizo, Bwana Mungu alipozifanya nchi na mbingu, 5miti yote ya mashambani ilikuwa haijawa bado, nazo mboga zote za mashambani zilikuwa hazijaota bado, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyesha bado mvua katika nchi, tena hakuwako mtu wa kulima shamba. 6Lakini kungugu lilipopanda toka nchini likanywesha upande wa nje wa nchi yote. 7Naye Bwana Mungu alipomwumba mtu alimtengeneza na kutumia mavumbi ya nchi, kisha akampulizia puani mwake pumzi ya uzima; ndipo, mtu alipopata kuwa mwenye roho ya uzima.#1 Kor. 15:45. 8Kisha Bwana Mungu akapanda shamba huko Edeni upande wa maawioni kwa jua; ndiko, alikomweka huyo mtu, aliyemwumba. 9Bwana Mungu akaichipuza nchi miti yote ipendezayo kwa kutazamwa nayo ifaayo kwa kuliwa, napo hapo katikati ya shamba mti wa uzima na mti wa kujulia mema na mabaya.#1 Mose 3:22,24; Ufu. 2:7; 22:2. 10Tena kule Edeni kulitoka jito la kulinywesha hilo shamba, likajigawanya papo hapo shambani kuwa makono manne. 11Jina lake mto wa kwanza ni Pisoni, uliizunguka nchi yote ya Hawila iliyokuwa na dhahabu. 12Nayo dhahabu ya nchi hii ilikuwa nzuri; tena kulikuwako magwede na vito vya oniki. 13Jina lake mto wa pili ni Gihoni, nao ndio ulioizunguka nchi yote ya Kusi. 14Jina lake mto wa tatu ni Hidekeli, nao ndio unaopita upande wa maawioni kwa jua wa nchi ya Asuri. Nao mto wa nne ndio Furati. 15Bwana Mungu akamchukua Adamu, akamkalisha katika shamba la Edeni, alilime na kuliangalia.
Agizo la Mungu.
16Kisha Bwana Mungu akamwagiza Adamu kwamba: Miti yote iliyomo humu shambani utaila,#Rom. 5:12; 1 Kor. 15:21. 17lakini mti wa kujulia mema na mabaya usiule! Kwani siku, utakapoula, huna budi kufa.
Kumwumba mkewe Adamu.
18Bwana Mungu akasema: Hiafai, mtu akiwa peke yake, nitamfanyizia mwenziwe wa kusaidiana naye. 19Bwana Mungu alipokwisha kuwatokeza katika nchi nyama wote wa porini na ndege wote wa angani akawapeleka kwa Adamu, aone, atakavyowaita; jina lake kila nyama mwenye uzima liwe lilo hilo, Adamu atakalomwita.#Fano. 31:10-31. 20Adamu akampa kila nyama wa nyumbani na kila ndege wa angani na kila nyama wa porini jila lake, lakini yeye Adamu hakuona mtu mwenziwe wa kusaidiana naye. 21Ndipo, Bwana Mungu alipomtia Adamu usingizi mzito, akalala usingizi kabisa. Kisha akamtoa ubavu wake mmoja, napo mahali pake akapaziba na nyama. 22Huo ubavu, aliomtoa Adamu, Bwana Mungu akauumba kuwa mke, akampeleka kwake Adamu.#1 Kor. 11:7-9,12; 1 Tim. 2:13. 23Adamu akasema: Kweli huyu ni mfupa utokao katika mifupa yangu, ni mwenye mwili utokao mwilini mwangu; kwa hiyo ataitwa mwanamke, kwa kuwa ametolewa katika mwanamume. 24Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake, agandamiane na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 25Nao wote wawili, Adamu na mkewe, walikuwa wenye uchi, lakini hawakuona soni.
Attualmente Selezionati:
1 Mose 2: SRB37
Evidenziazioni
Condividi
Copia
Vuoi avere le tue evidenziazioni salvate su tutti i tuoi dispositivi?Iscriviti o accedi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.