Лого на YouVersion
Икона за пребарување

Mwa 5

5
Wazawa wa Adamu
1 # 1 Nya 1:1; Mt 1:1; Lk 3:38; Efe 4:24; Kol 3:10; Mwa 1:27-28 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2#Mt 19:4; Mk 10:6mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. 4Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 5#Mwa 3:19; Ayu 30:23; Zab 49:7-9; 89:48; Rum 5:12; 1 Kor 15:21; Ebr 9:27Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
6Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi. 7Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. 8Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
9Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. 11Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
12Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. 14Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
15Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. 17Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
18 # 1 Nya 1:3; Amu 14:15 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 19Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. 20Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
21Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22#Mwa 17:1; 2 Fal 20:3; Zab 16:8; Mik 6:8; Mal 2:6; 1 The 2:12Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 23Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 24#2 Fal 2:11; Ebr 11:5; Yud 1:14Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
25Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. 26Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. 27Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
28Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. 29#Mwa 3:17; 4:11Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. 30Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. 31Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
32Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.

Селектирано:

Mwa 5: SUV

Нагласи

Сподели

Копирај

None

Дали сакаш да ги зачуваш Нагласувањата на сите твои уреди? Пријави се или најави се