1 Mose 14
14
Vita vya wafalme wanne.
1Ikawa siku zile za Amurafeli, mfalme wa Sinari, ndipo, yeye na Arioki, mfalme wa Elasari, na Kedori-Laomeri, falme wa Elamu, na Tidali, mfalme wa Goyimu, 2wakaenda kupiga vita na Bera, mfalme wa Sodomu, na Birsa, mfalme wa Gomora na Sinabu, mfalme wa Adima, na Semeberi, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela unaoitwa Soari. 3Hawa wote wakajiunga, wakakutana bondeni kwa Sidimu kwenye Bahari ya Chumvi. 4Kwani wale walimtumikia Kedori-Laomeri miaka kumi na miwili, lakini katika mwaka wa kumi na tatu walimvunjia maagano. 5Kwa hiyo Kedori-Laomeri na wafalme waliokuwa naye wakaja katika mwaka wa kumi na nne, wakawapiga wale Majitu kule Astaroti-Karnaimu nao Wazuzi kule Hamu nao Waemi katika nchi ya tambarare ya Kiriataimu, 6nao Wahori milimani kwao Seiri mpaka Eli-Parani ulioko upande wa nyikani. 7Kisha wakarudi, wakafika kwenye chemchemi ya Misipati, ndio Kadesi, wakaipiga nchi yote ya Waamaleki nao Waamori waliokaa Hasasoni-Tamari. 8Ndipo, walipotoka, mfalme wa Sodomu na mfalme wa Gomora na mfalme wa Adima na mfalme wa Seboimu na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakajipanga katika bonde la Sidimu kupigana. 9Nao wa Kedori-Laomeri, mfalme wa Elamu, na Tidali, mfalme wa Goyimu, na Amurafeli, mfalme wa Sinari, na Arioki, mfalme wa Elasari, walikuwa wafalme wanne, nao wale ni watano. 10Nako kule bondeni kwa Sidimu kulikuwa na mashimo mengi ya lami, nao wafalme wa Sodomu na wa Gomora walipokimbizwa wakatumbukia mlemle, nao watu waliosalia wakakimbilia milimani. 11Ndipo, walipoyateka mapato yote ya Sodomu na ya Gomora, navyo vilaji vyao vyote, wakaenda zao. 12Naye Loti, mwana wa nduguye Aburamu, wakamteka na mapato yake, wakenda zao, kwani alikaa Sodomu.#1 Mose 13:10-12.
Aburamu anamwokoa Loti.
13Mtu mmoja aliyejiponya akaja, akamsimulia Mwebureo Aburamu yaliyokuwa; naye alikuwa akikaa katika kimwitu cha Mwamori Mamure aliyekuwa ndugu yao Eskoli na Aneri, nao hao walikuwa wamefanya maagano na Aburamu. 14Aburamu aliposikia, ya kuwa ndugu yake ametekwa, akawachukua wazalia wa nyumbani mwake 318 waliozijua kazi za vita, akapiga mbio akiwafuata mpaka Dani. 15Usiku akawagawanya watu wake, akawashambulia, akawapiga; kisha akawakimbiza mpaka Hoba ulioko kushotoni kwa Damasko. 16Akayarudisha yale mapato yote, naye ndugu yake Loti akamrudisha pamoja na mapato yake, nao wanawake wa watu waliotekwa. 17Aliporudi kwa kumpiga Kedori-Laomeri na wale wafalme waliokuwa naye, mfalme wa Sodomu akatoka kumwendea njiani kule bondeni kwa Sawe, ndio bondeni kwa Mfalme.
Melkisedeki anambariki Aburamu.
18Naye Melkisedeki, mfalme wa Salemu, akamotolea mkate na mvinyo, naye alikuwa mtambikaji wa Mungu alioko huko juu.#Sh. 110:4; Ebr. 7:1-4,18; Sh. 76:3. 19Akambariki na kusema: Aburamu na atukuzwe kwa kuwa wake Mungu, mwenye mbingu naa nchi! 20Atukuzwe naye Mungu alioko huko juu, kwa kuwa amewatia adui zako mkononi mwako! Ndipo Aburamu alipompa fungu la kumi la mali zote, alizokuwa nazo. 21Kisha mfalme wa sodomu akamwambia Aburamu: Nipe watu wangu tu, mali uzitwae wewe. 22Lakini Aburamu akamwambia mfalme wa Sodomu: Mkono wangu namnyoshea Bwana Mungu alioko huko juu, aliye mwenye mbingu na nchi, kwamba: 23Katika mali zote zilizo zako sitachukua uzi wala kikanda tu cha kiatu, usiseme: Aburamu mali zake nyingi nimempa mimi. 24Hawa vijana tu wape chakula chao! Nao waume hawa waliokwenda pamoja nami, Aneri na Eskoli na Mamure, wao na wayachukue mafungu yao!
Obecnie wybrane:
1 Mose 14: SRB37
Podkreślenie
Udostępnij
Kopiuj
Chcesz, aby twoje zakreślenia były zapisywane na wszystkich twoich urządzeniach? Zarejestruj się lub zaloguj
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: