1 Mose 15
15
Aburamu anakitegemea kiagio, Mungu anachompa.
1Mambo hayo yalipomalizika neno la Bwana likamjia Aburamu katika ndoto kwamba: Usiogope Aburamu! Mimi ni ngao yako, nao mshahara wako ni mwingi.#Sh. 3:4; 84:12; 119:114. 2Aburamu akasema: Bwana Mungu, utanipa nini? Mimi ninajikalia pasipo mwana. Mwenye mali zilizomo nyumbani mwangu atakuwa huyu Eliezeri wa Damasko. 3Kisha Aburamu akasema: Hukunipa mzao; kwa hiyo atakayezichukua mali zangu ni mzalia wa nyumbani mwangu. 4Ndipo, neno la Bwama lilipomjia tena kwamba: Huyu hatazichukua mali zako; ila atakyetoka mwilini mwako ndiye atakayezichukua mali zako. 5Kisha akamtoa nje, akamwambia: Tazama juu mbinguni, uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu! Akamwambia: Hivi ndivyo, wao wa uzao wako watakavyokuwa wengi.#1 Mose 22:17; 2 Mose 32:13; 5 Mose 1:10. 6Naye akamtegemea Bwana, kwa hiyo akamwazia kuwa mwenye wongofu.#Rom. 4:3-5,18-22; Yak. 2:23.
Mungu anafanya maagano na Aburamu.
7Kisha akamwambia: Mimi ni Bwana, nimekutoa kule Uri wa Wakasidi, nikupe nchi hii, uichukue kuwa yako.#1 Mose 11:31. 8Naye akamwuliza: Bwana Mungu, nitajua namna gani, ya kuwa nitaichukua kuwa yangu?#2 Fal. 20:8; Luk. 1:18. 9Akamwambia: Nipatie mori wa miaka mitatu na mbuzi jike wa miaka mitatu na dume la kondoo wa miaka mitatu na hua na kinda la njiwa!#Yer. 34:18-19. 10Alipokwisha kumpatia hao wote, akawapasua kati, akayaweka manusu ya kila nyama upande upande, yaelekeane, lakini ndege hakuwapasua. 11Ngusu walipoishukia ile mizoga, Aburamu akawaamia. 12Lakini jua lilipoingia, usingizi mzito ukampata Aburamu, mara akastushwa na giza kuu lililomguia.#Iy. 4:13-14. 13Ndipo, Bwana alipomwambia Aburamu: Na ujue kabisa, ya kuwa wao wa uzao wako watakaa ugenini katika nchi isiyo yao, nao watawatumikia wenyeji, hao watawatesa miaka 400.#2 Mose 12:40; Tume. 7:6. 14Nao wale wamizimu, ambao watawatumikia, mimi nitawahukumu, kisha wao watapata kutoka wenye mapato mengi.#2 Mose 3:21-22. 15Lakini wewe utakwenda zako na kutengemana kwao baba zako, uzikwe utakapokwisha kuwa mzee wa miaka mingi. 16Nao watakaokuwa wa kizazi cha nne watarudi huku, kwa kuwa uovu wa Waamori haujatimia bado mpaka sasa. 17Jua lilipokwisha kuingia, kukawa na giza jeusi sana, mara likawa kama moshi wa tanuru wenye miali ya moto iliyopita katikati ya vile vipande vya nyama.
18Hivyo ndivyo, Bwana alivyofanya siku hiyo maagano na Aburamu kwamba: Nchi hii nitwapa wao wa uzao wako toka lile jito la Misri mpaka lile jito kubwa, lile jito la Furati,#1 Mose 12:7. 19kwao Wakeni na Wakenizi na Wakadimoni,#1 Mose 10:15-18. 20na Wahiti na Waperizi na wale Majitu, 21na Waamori na Wakanaani na Wagirgasi na Wayebusi.#4 Mose 13:33.
Obecnie wybrane:
1 Mose 15: SRB37
Podkreślenie
Udostępnij
Kopiuj
Chcesz, aby twoje zakreślenia były zapisywane na wszystkich twoich urządzeniach? Zarejestruj się lub zaloguj
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: