1
Mwanzo 12:2-3
Biblia Habari Njema
Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka. Anayekubariki, nitambariki; anayekulaani, nitamlaani. Kwako wewe, nitayabariki mataifa yote ya dunia.”
Comparar
Explorar Mwanzo 12:2-3
2
Mwanzo 12:1
Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, acha jamaa yako na nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayokuonesha.
Explorar Mwanzo 12:1
3
Mwanzo 12:4
Kwa hiyo, Abramu akaondoka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru; na Loti akaenda pamoja naye. Abramu alikuwa na umri wa miaka 75 alipotoka Harani.
Explorar Mwanzo 12:4
4
Mwanzo 12:7
Ndipo Mwenyezi-Mungu akamtokea Abramu, akamwambia, “Wazawa wako nitawapa nchi hii.” Basi, Abramu akajenga madhabahu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu aliyemtokea.
Explorar Mwanzo 12:7
Início
Bíblia
Planos
Vídeos