Yohana 2
2
Arusi iliyokuwako Kana.
1*Siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya arusi huko Kana wa Galilea, hata mamake Yesu alikuwako, 2naye Yesu na wanafunzi wake wakaalikwa arusini. 3Mvinyo ilipopunguka, mamake Yesu akamwambia: Hawana mvinyo. 4Yesu akamwambia: Mama, tuko na jambo gani, mimi na wewe? Saa yangu haijaja bado.#Yoh. 19:26; Mat. 12:48. 5Ndipo, mama yake alipowaambia watumishi: Lo lote atakalowaambia, lifanyeni! 6Pale palikuwa na mitungi sita ya mawe iliyokuwa imewekwa kwa desturi ya kunawa kwao Wayuda; kila mmoja ulienea mabuyu mawili au matatu.#Mar. 7:3-4. 7Yesu akawaambia: Ijazeni mitungi maji! Walipokwisha kuijaza mpaka juu, 8akawaambia: Sasa tekeni, mmpelekee mwandaliaji! Basi, wakampelekea. 9Lakini mwandaliaji hakujua, ilikotoka, watumishi tu waliokuwa wameyateka yale maji walijua. Mwandaliaji alipoyaonja yale maji yaliyogeuka kuwa mvinyo akamwita bwana arusi, 10akamwambia: Kila mtu hutoa kwanza mvinyo nzuri; watu wakiisha kushiba, huileta isiyo nzuri sana; lakini wewe iliyo nzuri umeiweka mpaka sasa. 11Huo ndio mwanzo wa vielekezo, Yesu alivyovifanya, nao ulifanyika Kana wa Galilea; ndivyo, alivyoufunua utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamtegemea.*#Yoh. 1:14.
12Kisha wakashuka kwenda Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake, wakakaa huko siku zisizokuwa nyingi.#Yoh. 7:3.
Kuwafukuza wachuuzi Patakatifu.
13*Pasaka ya Wayuda ilipokuwa karibu, Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.
(14-16: Mat. 21:12-13; Mar. 11:15-17; Luk. 19:45-46.)
14Alipoona hapo Patakatifu wenye kuuzia palepale ng'ombe na kondoo na njiwa, hata wavunjaji wa fedha waliokuwapo wamekaa, 15akaokota kamba, akazisuka kambaa, akawafukuza wote hapo Patakatufu, hata kondoo na ng'ombe, akazimwaga fedha za wavunjaji na kuziangusha meza zao. 16Wenye kuuza njiwa akawaambia: Yaondoeni haya hapa! Msiigeuze Nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya uchuuzi! 17Hapo wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa imeandikwa:#Sh. 69:10.
18Kwa ajili ya Nyumba yako wivu unanila!* Wayuda walipomwuliza wakimwambia: Unatuonyesha kielekezo gani, kwa kuwa unafanya hivyo?#Mat. 21:23. 19Yesu akajibu akiwaambia: Livunjeni Jumba hili la Mungu! Nami nitalijenga tena muda wa siku tatu.#Mat. 26:61; 27:40. 20Wayuda wakasema: Jumba hili la Mungu lilijengwa kwa miaka 46, nawe utalijenga kwa siku tatu? 21Lakini yeye alilisema Jumba la Mungu lililo mwili wake.#1 Kor. 6:19. 22Hapo, alipokwisha kufufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa aliyasema hayo. Wakayategemea Maandiko na neno hilo, Yesu alilolisema.
23Lakini alipokuwako Yerusalemu siku za sikukuu ya Pasaka, wengi wakaja kulitegemea Jina lake walipoviona vielekezo vyake, alivyovifanya. 24Lakini Yesu mwenyewe hakuwategemea, kwamba wanamtegemea, kwani yeye aliwatambua wote; 25kwa hiyo hakutaka kushuhudiwa na mwingine mambo ya mtu, maana aliyatambua mwenyewe yaliyomo moyoni mwa mtu.#Mar. 2:8.
Trenutno izabrano:
Yohana 2: SRB37
Istaknuto
Podijeli
Kopiraj
Želiš li da tvoje istaknuto bude sačuvano na svim tvojim uređajima? Kreiraj nalog ili se prijavi
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.