Mattayo MT. 23

23
1KIISHA Yesu akasema na makutano na wanafunzi wake, akinena, 2Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa: 3bassi, yo yote watakayowaambieni myashike; yashikeni na kuyatenda: lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende: maana hunena wala hawatendi. 4Kwa maana hufunga mizigo mizito isiyochukulika na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuisogeza kwa kidole chao. 5Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao; 6hupenda mahali pa mbele katika karamu, na viti vya mbele katika sunagogi, 7na kusalimiwa sokoni, na kuitwa na watu, Rabbi, Rabbi. 8Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu. 9Wala msimwite mtu baba yenu duniani: maana Baba yeuu yu mmoja, aliye mbinguni. 10Wala msiitwe wakufunzi; maana mkufunzi wenu yu mmoja, ndiye Kristo. 11Nae aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. 12Na ye yote atakaejikuza, atadhiliwa; na ye yote atakaejidhili, atakuzwa.
13Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.
14Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, nao wanaoingia hamwaachi waingie.
15Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.
16Ole wenu viongozi vipofu, ninyi mnenao, Mtu atakaeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa dhababu ya hekalu, amejifunga. 17Wapumbavu ninyi na vipofu: maana ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhababu? 18Tena, Mtu atakaeapa kwa madhbahu, si kitu; bali mtu atakaeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ipi kubwa, ile sadaka, au ile madhbahu iitakasayo sadaka? 20Bassi yeye aapae kwa madhbahu, yuapa kwayo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21Nae aapae kwa hekalu, yuapa kwalo, na kwa yeye akaae ndani yake. 22Nae aapae kwa mbingu, yuapa kwa kiti cha Mungu, na kwa yeye akaae juu yake.
23Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnaana na bizari na kumini, mkaacha mambo makuu ya sharia, hukumu, na rehema, na imani: haya imewapasa kuyafanya, na mengine yale msiyaache. 24Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.
25Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi. 26Ewe Farisayo kipofu, takasa kwanza ndani ya kikombe na chungu, illi nje yake nayo ipate kuwa safi.
27Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa yamepambwa, bali kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. 28Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, hali kwa ndani mmejaa unafiki na maasi.
29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki? kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30na kunena, Kama sisi tungalikuwako zamani za haha zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31Hivi mwajishuhudia nafsi zenu, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowana manabii. 32Kajazeni kipimo cha baba zenu. 33Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum? 34Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji; 35illi iwajieni damu yote ya haki iliyomwagika katika inchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hatta damu ya Zakaria, mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhbahu, 36Amin, nawaambieni, Mambo haya yote yatakijia kizazi hiki.
37Ee Yerusalemi, Yerusalemi, wenye kuwaua manabii, na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkukubali! 38Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa tupu. 39Kwa maana nawaambieni, Hamtaniona kamwe tangu leo, hatta mtakaposema, Ameharikiwa ajae kwa jina la Bwana.

Märk

Dela

Kopiera

None

Vill du ha dina höjdpunkter sparade på alla dina enheter? Registrera dig eller logga in