1
Wagalatia 6:9
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.
Linganisha
Chunguza Wagalatia 6:9
2
Wagalatia 6:10
Kwa hiyo, kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema, hasa wale wa jamaa ya waumini.
Chunguza Wagalatia 6:10
3
Wagalatia 6:2
Chukulianeni mizigo ninyi kwa ninyi, nanyi kwa njia hii mtatimiza sheria ya Al-Masihi.
Chunguza Wagalatia 6:2
4
Wagalatia 6:7
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Chunguza Wagalatia 6:7
5
Wagalatia 6:8
Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho wa Mungu, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Chunguza Wagalatia 6:8
6
Wagalatia 6:1
Ndugu zangu, ikiwa mtu amepatikana akitenda dhambi, basi ninyi mnaoishi kwa Roho wa Mungu mnapaswa kumrejesha mtu huyo kwa upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa.
Chunguza Wagalatia 6:1
7
Wagalatia 6:3-5
Mtu yeyote akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe sivyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine. Kwa maana, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
Chunguza Wagalatia 6:3-5
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video