Ndipo akambariki Yusufu akisema,
“Mungu ambaye baba zangu
Ibrahimu na Isaka walimtii,
Mungu ambaye amekuwa mchungaji
wa maisha yangu yote hadi leo,
Malaika ambaye aliniokoa kutoka madhara yote,
yeye na awabariki vijana hawa.
Na waitwe kwa jina langu
na kwa majina ya baba zangu
Ibrahimu na Isaka,
wao na waongezeke kwa wingi
katika dunia.”