1
Waebrania 1:3
Neno: Bibilia Takatifu
Mwana ni mngʼao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
Linganisha
Chunguza Waebrania 1:3
2
Waebrania 1:1-2
Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu.
Chunguza Waebrania 1:1-2
3
Waebrania 1:14
Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?
Chunguza Waebrania 1:14
4
Waebrania 1:10-11
Pia asema, “Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu; zote zitachakaa kama vazi.
Chunguza Waebrania 1:10-11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video