1
Isaya 1:18
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
“Njooni basi tujadiliane,” asema Mwenyezi Mungu. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.
Linganisha
Chunguza Isaya 1:18
2
Isaya 1:19
Mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi
Chunguza Isaya 1:19
3
Isaya 1:17
Jifunzeni kutenda mema, tafuteni haki. Wateteeni waliodhulumiwa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.
Chunguza Isaya 1:17
4
Isaya 1:20
lakini mkikataa na kuasi, mtaangamizwa kwa upanga.” Kwa kuwa kinywa cha Mwenyezi Mungu kimenena.
Chunguza Isaya 1:20
5
Isaya 1:16
“Jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele zangu; acheni kutenda mabaya.
Chunguza Isaya 1:16
6
Isaya 1:15
Mnaponyoosha mikono yenu katika maombi, nitaficha macho yangu nisiwaone; hata mkiomba maombi mengi sitasikiliza. “Mikono yenu imejaa damu!
Chunguza Isaya 1:15
7
Isaya 1:13
Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana! Uvumba wenu ni chukizo kwangu. Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada: siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.
Chunguza Isaya 1:13
8
Isaya 1:3
Ng’ombe anamjua bwana wake, naye punda anajua hori la mmiliki wake, lakini Israeli hajui, watu wangu hawaelewi.”
Chunguza Isaya 1:3
9
Isaya 1:14
Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi, na sikukuu zenu zilizoamriwa: moyo wangu unazichukia kabisa. Zimekuwa mzigo kwangu, nimechoka kuzivumilia.
Chunguza Isaya 1:14
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video