1
Yeremia 50:34
Neno: Bibilia Takatifu
Lakini Mkombozi wao ana nguvu; BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.
Linganisha
Chunguza Yeremia 50:34
2
Yeremia 50:6
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzurura juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
Chunguza Yeremia 50:6
3
Yeremia 50:20
Katika siku hizo, wakati huo,” asema BWANA, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
Chunguza Yeremia 50:20
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video