Jua na mwezi vitatiwa giza,
na nyota hazitatoa mwanga wake tena.
Mwenyezi Mungu atanguruma kutoka Sayuni
na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;
dunia na mbingu vitatikisika.
Lakini Mwenyezi Mungu atakuwa kimbilio la watu wake,
ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.