1
Marko 16:15
BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA
Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu.
Linganisha
Chunguza Marko 16:15
2
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”
Chunguza Marko 16:17-18
3
Marko 16:16
Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa.
Chunguza Marko 16:16
4
Marko 16:20
Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao.]
Chunguza Marko 16:20
5
Marko 16:6
Lakini huyo kijana akawaambia, “Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwa wamemlaza.
Chunguza Marko 16:6
6
Marko 16:4-5
Lakini walipotazama, waliona jiwe limekwisha ondolewa. (Nalo lilikuwa kubwa mno.) Walipoingia kaburini, walimwona kijana mmoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wa kulia; wakashangaa sana.
Chunguza Marko 16:4-5
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video