Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja? Ulipokuwa kwako, haukuwa mali yako? Na ulipokuwa umekwisha kuuzwa haukuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hatta ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uwongo mwana Adamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Khofu nyiugi ikawapata watu wote walioyasikia haya.