1
Mattayo MT. 22:37-39
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Amri ya kwanza na iliyo kuu ndiyo hii. Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Linganisha
Chunguza Mattayo MT. 22:37-39
2
Mattayo MT. 22:40
Amri hizi mbili yazitegemea torati yote nao manabii.
Chunguza Mattayo MT. 22:40
3
Mattayo MT. 22:14
Kwa maana wengi waitwao, wateule wachache.
Chunguza Mattayo MT. 22:14
4
Mattayo MT. 22:30
Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaozwi, bali huwa kama malaika wa Mungu mbinguni.
Chunguza Mattayo MT. 22:30
5
Mattayo MT. 22:19-21
Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. Akawaambia, Ya nani sanamu hii, na anwani hii? Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Chunguza Mattayo MT. 22:19-21
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video