Siku zile Mose alipokwisha kukua akatoka kwenda kwa ndugu zake; alipovitazama, walivyofanyishwa kazi ngumu, akaona Mmisri mmoja, akimpiga mmoja wao ndugu zake wa Kiebureo. Ndipo, alipogeuka huko na huko, tena alipoona, ya kama hakuna mtu, akampiga yule Mmisri na kumwua, kisha akamfukia mchangani.