“Wakati waja kwa hakika,
ambapo mara baada ya kulima
mavuno yatakuwa tayari kuvunwa;
mara baada ya kupanda mizabibu
utafuata wakati wa kuvuna zabibu.
Milima itabubujika divai mpya,
navyo vilima vitatiririka divai.
Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli.
Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo;
watapanda mizabibu na kunywa divai yake;
watalima mashamba na kula mazao yake.