Hivi ndivyo asemavyo Mungu aliye juu kabisa,
aishiye milele na ambaye jina lake ni “Mtakatifu”:
“Mimi nakaa huko juu, mahali patakatifu,
nakaa pia na wenye majuto na wanyenyekevu.
Mimi nitawatia moyo walio wanyenyekevu
na kuwapa nguvu wenye majuto.
Maana sitaendelea kuwalaumu
wala kuwakasirikia daima.
La sivyo hao niliowaumba watadhoofika mbele yangu,
nami ndiye niliyewapa pumzi yangu ya uhai.