“Kama ukiacha kufanya kazi siku ya Sabato,
ukaacha shughuli zako siku yangu hiyo takatifu;
kama ukiifanya siku yangu kuwa ya furaha,
ukaiheshimu siku hiyo takatifu ya Mwenyezi-Mungu,
ukaacha na shughuli zako na kupiga domo,
utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu,
nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini,
nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako.
Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”