1 Wakorintho 1:4-9
1 Wakorintho 1:4-9 NENO
Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Al-Masihi Isa. Kwa kuwa katika Al-Masihi mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Al-Masihi ulithibitishwa ndani yenu. Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi. Atawafanya imara hadi mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Isa Al-Masihi. Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Isa Al-Masihi, Bwana wetu ni mwaminifu.