Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 14:20-25

1 Wakorintho 14:20-25 NENO

Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima. Katika Torati imeandikwa kwamba: “Kupitia kwa watu wenye lugha ng’eni na kupitia midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Mwenyezi Mungu.” Basi kunena kwa lugha ni ishara, si kwa waaminio, bali kwa wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio. Kwa hiyo kama kundi la waumini wote wakikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioelewa au wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu? Lakini kama mtu asiyeamini au asiyeelewa akiingia wakati kila mtu anatoa unabii, ataaminishwa na watu wote kuwa yeye ni mwenye dhambi na kuhukumiwa na wote, nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko kati yenu!”