1 Wakorintho 3:16-23
1 Wakorintho 3:16-23 NENO
Je, hamjui kwamba ninyi wenyewe ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu yeyote akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamwangamiza; kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ndio hilo hekalu. Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima. Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kama ilivyoandikwa: “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao,” tena, “Mwenyezi Mungu anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.” Hivyo basi, mtu asijivune kuhusu wanadamu! Vitu vyote ni vyenu, iwe ni Paulo au Apolo au Kefa, au dunia au uzima au mauti, au wakati uliopo au ujao: haya yote ni yenu, na ninyi ni wa Al-Masihi, naye Al-Masihi ni wa Mungu.