Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 11:9-13

1 Wafalme 11:9-13 NEN

BWANA akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili. Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya BWANA. Kwa hiyo BWANA akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako. Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Wafalme 11:9-13