Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 2:26-35

1 Wafalme 2:26-35 NENO

Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la Bwana Mungu Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.” Hivyo Sulemani akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Mwenyezi Mungu, akilitimiza neno la Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli. Habari zilipomfikia Yoabu, aliyekuwa amepanga njama na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu na kushika pembe za madhabahu. Mfalme Sulemani akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la Mwenyezi Mungu naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Sulemani akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!” Ndipo Benaya akaingia kwenye hema la Mwenyezi Mungu na kumwambia Yoabu, “Mfalme anasema, ‘Toka nje!’ ” Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.” Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo Yoabu alivyonijibu.” Kisha mfalme akamwamuru Benaya, “Fanya kama asemavyo. Muue na kumzika, ili uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu aliyoimwaga. Mwenyezi Mungu atamlipiza kwa ajili ya damu aliyoimwaga, kwa sababu pasipo Daudi baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda, walikuwa watu wazuri na wanyofu kuliko yeye. Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Mwenyezi Mungu milele.” Basi Benaya mwana wa Yehoyada akakwea, akamgonga na kumuua Yoabu, naye akazikwa katika shamba lake mwenyewe jangwani. Mfalme akamweka Benaya mwana wa Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu, na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari.