Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme 9:24-28

1 Wafalme 9:24-28 NEN

Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Solomoni alikuwa amemjengea, akajenga Milo. Solomoni akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya BWANA, akifukiza uvumba mbele za BWANA pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu. Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu. Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Solomoni. Wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri na kurudi na talanta 420 za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Wafalme 9:24-28