Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro Utangulizi

Utangulizi
Petro ni mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Aliandikia waraka huu kwa Wakristo wa Kiyahudi wa Utawanyiko waliokuwa Asia Ndogo. Waraka huu unaonyesha kwamba waumini walikuwa wanakabiliwa na dhiki na mateso. Lengo lake lilikuwa kuwafariji waumini waliokuwa wakiishi Asia, kwani katika kipindi hiki cha miaka ya sitini ya karne ya kwanza, utawala wa Rumi chini ya Nero ulianza kuwatesa Wakristo.
Kwa wale waliokuwa wakifikiria kurudia imani yao ya Kiyahudi ili kuepuka mateso, anawaambia kuwa sasa kanisa ndilo ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki yake Mungu. Hivyo mawazo ya kurejea imani ya Kiyahudi hayana faida yoyote. Kisha Petro anatoa mfano wa Kristo na jinsi alivyopata mateso, na anawakumbusha waumini kuwa wao pia hawana budi kupata mateso. Mwishowe, Petro anatoa maagizo kwa vikundi mbalimbali vya Wakristo.
Mwandishi
Mtume Petro.
Kusudi
Kuwatia moyo Wakristo kusimama dhabiti katika mateso yote, na kuwa imara katika neema ya Mungu.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Kama 63 B.K.
Wahusika Wakuu
Petro, Silvano, na Marko.
Wazo Kuu
Hata kama tutauawa kwa ajili ya imani, tushikilie imani yetu. Mungu anafahamu yote yanayotendeka, na katika mpango wake wa milele, hatimaye mambo yote yatakamilika kwa utukufu wake.
Mambo Muhimu
Petro anaonyesha kwamba mateso ni sehemu ya maisha ya Kikristo, na kwamba Mungu ameandaa thawabu zisizoharibika kwa wote wanaomwamini. Pia anaonyesha tumaini la wakati wa mwisho kuwa jambo la kumtia moyo muumini katika mateso.
Mgawanyo
Utukufu wa wokovu wa Kristo (1:1-25)
Utiifu wa Mkristo (2:1-10)
Mfano wa mateso ya Kristo (2:11-25)
Maisha yampasayo Mkristo (3:1-17)
Mateso na mfano wa Kristo (3:18–4:19)
Huduma ya Kikristo, na mawaidha ya mwisho (5:1-14).

Iliyochaguliwa sasa

1 Petro Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia