Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli Utangulizi

Utangulizi
Katika andiko la Kiebrania, vitabu vya 1 Samweli na 2 Samweli vilikuwa kitabu kimoja. Kugawanyika na kuwa vitabu viwili kulifanyika katika tafsiri ya “Septuagint” (yaani Maandiko Matakatifu kwa Kiyunani), ambayo iliviita “Kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Ufalme.” Kitabu cha 1 Samweli kinaanza kuelezea kuzaliwa kwa Samweli na mafundisho yake hekaluni. Kinaelezea jinsi alivyoiongoza Israeli kama nabii, kuhani na mwamuzi.
Waisraeli walipotamani kuwa na mfalme, Samweli, kwa uongozi wa Mwenyezi Mungu, alimtia Sauli mafuta kuwa mfalme wa kwanza wa Waisraeli. Lakini Sauli aliacha kumtii Mwenyezi Mungu, naye Mungu akamkataa asiendelee kuwa mfalme. Kisha Mwenyezi Mungu akamwongoza Samweli kumtia Daudi mafuta kwa siri kuwa mfalme mahali pa Sauli. Sehemu ya kitabu hiki iliyobaki inaelezea mapambano kati ya Sauli na Daudi.
Mwandishi
Inawezekana ni Samweli hadi mahali kifo chake kimenakiliwa; pia maandishi ya manabii Nathani na Gadi yamejumuishwa.
Kusudi
Kitabu cha 1 Samweli kinaonesha historia ya Israeli chini ya uongozi wa waamuzi, kuonesha mabadiliko ya uongozi katika Israeli kutoka mfumo wa uongozi wa waamuzi kwenda kwa uongozi wa wafalme, na kuweka kumbukumbu za maisha ya watu ambao kupitia kwao Masihi angezaliwa.
Mahali
Katika nchi ya Israeli.
Tarehe
Wakati kitabu hiki kiliandikwa haujulikani.
Wahusika Wakuu
Eli, Hana, Samweli, Sauli, Yonathani, na Daudi.
Wazo Kuu
Kuanzishwa kwa ufalme wa Waisraeli, na vile huo ufalme uliendelea chini ya Mfalme Sauli na Daudi.
Mambo Muhimu
Kitabu cha 1 Samweli kinaonesha kumomonyoka kwa maadili kwa waamuzi wakati wa Samweli; mwanzo wa kushindwa kwa ufalme wakati wa Sauli; Daudi kutiwa mafuta na kujaribiwa kwa uzoefu wake; na pia, mwisho wa Sauli.
Yaliyomo
Eli, kuhani na mwamuzi, na Samweli (1:1–7:17)
Samweli na Sauli, viongozi wa Israeli (8:1–15:35)
Mfalme Sauli, na Daudi (16:1–31:13).

Iliyochaguliwa sasa

1 Samweli Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia