Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 1:18-20

1 Timotheo 1:18-20 NENO

Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri, ukiishikilia imani na dhamiri safi, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao. Miongoni mwao wako Himenayo na Iskanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.