Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Timotheo 5:1-8

1 Timotheo 5:1-8 NENO

Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako; nao wanawake wazee uwatendee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako, katika usafi wote. Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli. Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hawa inawapasa awali ya yote wajifunze kutimiza wajibu wao wa kumcha Mungu katika matendo kwa kuwatunza wale wa jamaa zao wenyewe, na hivyo wawarudishie wema waliowatendea wazazi wao, kwa kuwa hivi ndivyo inavyompendeza Mungu. Mwanamke ambaye ni mjane kweli kweli, yaani yeye aliyebaki peke yake huweka tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na mchana akimwomba Mungu ili amsaidie. Lakini mjane aishiye kwa anasa amekufa, ingawa anaishi. Wape watu maagizo haya pia, ili asiwepo yeyote wa kulaumiwa. Kama mtu hawatunzi wale wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani mwake mwenyewe, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.