Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Waraka wa pili wa Yohana uliandikwa kwa mama mteule na watoto wake. Unaweza kuwa ulimhusu mtu binafsi na jamaa yake, au ulilihusu kundi fulani la waumini. Msisitizo unawekwa katika umuhimu wa imani kwamba Isa ni Mwana wa Mwenyezi Mungu katika umbo la mwanadamu. Inawapasa waumini wanaosoma kudumu katika pendo la Mwenyezi Mungu, na kukataa mafundisho mapotovu yanayopinga imani ya kweli.
Yohana pia aliandika kuwaonya ili waweze kutambua walimu wa uongo waliosafiri kila mahali, wasije wakawaunga mkono na kuwasaidia. Yaani mtu yeyote asije akachangia kwenye kueneza mafundisho ya uongo badala ya yale ya kweli.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Kuhimiza mwenendo wa muumini, na maonyo kuhusu walimu wa uongo na mbinu zao.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Mnamo 90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana, mama mteule na watoto wake.
Wazo Kuu
Mtume Yohana anaagiza watu kuenenda katika kweli na kumtii Mwenyezi Mungu, wakijihadhari na walimu wa uongo, ili wapate kumpenda Mwenyezi Mungu, na kupendana wao kwa wao.
Mambo Muhimu
Pendo la kweli ni kuwajali wengine. Tunatamani kupendwa na kuwapenda wengine, lakini tunaona mifano michache sana ya uhalisi katika jambo hili. Dunia imejaa ubinafsi, uchoyo na kujipenda mwenyewe.
Yaliyomo
Salamu (1-3)
Kweli na upendo (4-11)
Salamu za mwisho (12-13).

Iliyochaguliwa sasa

2 Yohana Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia