Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 2:1-11

2 Samweli 2:1-11 NEN

Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamuuliza BWANA, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?” BWANA akasema, “Panda.” Daudi akauliza, “Je, niende wapi?” BWANA akajibu, “Nenda Hebroni.” Basi Daudi akakwea kwenda huko pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Pia Daudi akawachukua watu waliokuwa pamoja naye, kila mmoja na jamaa yake, nao wakaishi huko Hebroni na miji yake. Ndipo watu wa Yuda wakaja Hebroni, huko wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Daudi alipoambiwa kuwa ni watu wa Yabeshi-Gileadi waliomzika Sauli, akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi-Gileadi kuwaambia, “BWANA awabariki kwa kuonyesha wema huu kwa kumzika Sauli bwana wenu. Sasa BWANA na awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili. Sasa basi, kuweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.” Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu. Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Waasheri, Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote. Ish-Boshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi. Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Samweli 2:1-11