Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 5:17-25

2 Samweli 5:17-25 NEN

Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, kwa hiyo Daudi akamuuliza BWANA, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” BWANA akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.” Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu. Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua. Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. Kwa hiyo Daudi akamuuliza BWANA, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa BWANA ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” Basi Daudi akafanya kama BWANA alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba hadi Gezeri.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Samweli 5:17-25