Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Wathesalonike Utangulizi

Utangulizi
Waraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Isa. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Al-Masihi atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Mwenyezi Mungu, yaani siku ya hukumu, haingewafikia mara moja, bali ingetanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Al-Masihi angerudi, iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Isa Al-Masihi mara ya pili.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Mnamo 51–52 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Silvano na Timotheo.
Wazo Kuu
Kuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Kurudi kwa Isa Al-Masihi, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.
Yaliyomo
Faraja kutokana na kurudi kwa Al-Masihi (1:1-12)
Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Mwenyezi Mungu (2:1–3:5)
Mausia ya wafuasi wa Al-Masihi, na kuwatakia heri (3:6-18).

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia