Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo Utangulizi

Utangulizi
Huu ulikuwa waraka wa mwisho wa Paulo. Baada ya kuandika waraka wa kwanza kwa Timotheo msaidizi wake, Paulo alikamatwa na kurudishwa gerezani huko Rumi. Katika waraka huu, Paulo alimwambia Timotheo kwamba alihisi fursa zake za kuhubiri Injili zilikuwa zikifikia kikomo. Alimkumbusha Timotheo kwamba hata kama maisha yake hapa duniani yangekoma, Mwenyezi Mungu alikuwa amemwandalia maisha ya milele. Paulo pia alimkumbusha kuhusu uaminifu wa Mwenyezi Mungu ambaye alikuwa amemwongoza maisha yake yote. Aligusia nyakati za hatari ambazo zingekuja, na siku za taabu ambapo watu wangeiacha kweli na kupenda anasa kuliko kumpenda Mwenyezi Mungu.
Alijitahidi kumtia moyo Timotheo na kumwimarisha kwa ajili ya kazi kubwa aliyokabidhiwa. Paulo alitamani kumwona Timotheo tena, akimwomba amletee vile vitabu alivyokuwa ameviacha Troa.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kumpa maelekezo ya mwisho, na kumtia moyo Timotheo, mchungaji wa kundi la waumini la Efeso.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 66–67 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Timotheo, Luka, Marko.
Wazo Kuu
Barua hii inazungumzia uweza wa Mwenyezi Mungu juu ya vitu vyote. Ingawa kuna mateso ambayo yataendelea kuongezeka, Mwenyezi Mungu bado anatawala.
Mambo Muhimu
Kumwelekeza Timotheo ajitahidi kujionesha kuwa amekubalika na Mwenyezi Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, akilitumia kwa usahihi neno la kweli.
Yaliyomo
Salamu, na maagizo ya Paulo kwa Timotheo (1:1–2:13)
Sifa za mtumishi mwaminifu (2:14-26)
Hatari za siku za mwisho (3:1-17)
Maagizo ya mwisho (4:1-22).

Iliyochaguliwa sasa

2 Timotheo Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia