Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 33:23-29

Kumbukumbu 33:23-29 NENO

Kuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Mwenyezi Mungu, naye amejaa baraka yake; atarithi magharibi na kusini.” Kuhusu Asheri akasema: “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri; yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake, yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta. Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba, nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako. “Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni, ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie, na juu ya mawingu katika utukufu wake. Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’ Hivyo Israeli ataishi salama peke yake. Mzao wa Yakobo ni salama katika nchi ya nafaka na divai mpya, mahali mbingu hudondosha umande. Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na Mwenyezi Mungu? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”