Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhubiri Utangulizi

Utangulizi
Neno la Kiyunani “Ecclesiastes” limetafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania “Qoheleth.” Maana yake ni “Mhubiri” au “Yeye ahutubiaye kusanyiko.” Maadamu mwandishi anajitaja mwenyewe mara nyingi kuwa ndiye “Mhubiri.” Jina hili “Mhubiri” linaonekana kuwa ndilo linalofaa kukitambulisha kitabu hiki. Neno “Mwalimu” lililotumika katika tafsiri ya Agano la Kale ya Kiyunani “Septuagint” ndilo linalofanana na hili. Kitabu cha Mhubiri kinachunguza maana ya maisha.
Mwandishi
Solomoni.
Kusudi
Kusudi la kitabu hiki ni kuchunguza maisha kwa ujumla wake na kufundisha kwamba upembuzi wa mwisho unaonyesha kuwa maisha hayana maana, yaani ni ubatili, bila kumheshimu na kumcha Mungu kikamilifu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Kama mwaka wa 935 K.K.
Wahusika Wakuu
Solomoni.
Wazo Kuu
Ili kuelewa maisha na kufanya uamuzi ulio sawa, binadamu anahitaji hekima ambayo inapatikana kwa kumjua Mungu pekee.
Mambo Muhimu
Kuonyesha jinsi kufuata starehe maishani kunaweza kuleta udanganyifu wa dhambi na kutukosesha utoshelevu na furaha. Chanzo cha furaha, mafanikio na utoshelevu ni kumcha Mungu na kuzishika amri zake. Kama mtu yeyote ataishi na Mungu daima, basi kumtii Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha ya hapa duniani.
Mgawanyo
Maisha ni ubatili kabisa (1:1-11)
Kikomo cha hekima (1:12–2:26)
Wakati kwa kila jambo (3:1-22)
Ugumu wa maisha na kumcha Mungu (4:1–5:20)
Maudhi na kutosheka (6:1–8:17)
Maisha ni lazima yatawaliwe na hekima (9:1–10:20)
Hekima ya kweli ni kumcha Mungu (11:1–12:14).

Iliyochaguliwa sasa

Mhubiri Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia