Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 4:11-16

Waefeso 4:11-16 NENO

Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili mwili wa Al-Masihi upate kujengwa hadi sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima, kwa kufikia kimo cha ukamilifu wa Al-Masihi. Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho, na kwa ujanja na hila za watu katika njama zao. Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani Al-Masihi. Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeungamanishwa na kushikanishwa pamoja kwa msaada wa kila kiungo, hukua na kujijenga wenyewe katika upendo, huku kila kiungo kikifanya kazi yake.